Friday, March 30, 2012

Tabia na Mahusiano kwa Mkristo


SOMO: TABIA NA MAHUSIANO
Mafundisho
Na Mr.Gammariel Chiduo

TABIA 6 ZA LAZIMA KATIKA KUJENGA USHIRIKA AU MAHUSIANO MAZURI
NA MUNGU, MKE /MUME, JAMII AU WATU WOTE

UTANGULIZI
·       Mwanadamu sio kisiwa, lazima akutane na ashirikiane na watu wengine /au na Mungu
·       (Mwanzo 1:26) Mungu anajifunua kwetu katika ushirika “NA TUFANYE MTU…”
·       Kuumbwa kwetu ni katika kutimiza takwa la USHIRIKA.
·       Umeubwa kwa ajili ya wengine
  •  Mungu amekuumba hivyo ulivyo kwa ajili ya wengine 
  • Ndio maana tuko tofauti sana. Mungu hajacopy na kupaste.  
  • Tofauti zetu huleta hitaji la USHIRIKA na kushirikiana
  • Utajikuta chochote unachofanya ni kwa ajili ya watu wengine. Mfano:
-         Unavaa kwa ajili ya watu, ili watu watakapokuona waone umependeza. Kioo kitakusaidia. Kama ni kwaajili yako vaa suti, ukalale au kaa chumbani.
-         Uhai wako ni kwa ajili ya watu. Ukitaka kujinyonga utashtakiwa. Jaribu kuwaambia kuwa uhai ni wangu, sasa nataka kuutoa kama watakuelewa.
·       Utajikuta unalazimika kujenga ushirika na wengine maana unawahitaji, na wanakuhitaji sana, hivyo hivyo ulivyo wewe ni wa thamani sana!!
·       Umoja ni jambo muhimu sana katika maisha yetu ya wokovu (Yoh 17:20-24) Yesu anatuombea tuwe na umoja.
·       Umoja ni kati ya vitu vinavyopigwa vita sana na shetani – ndiko kuliko na siri ya nguvu na ushindi.
·       (Mithali 30:27) Nzige hawana mfalme, lakini huenda makundi makundi.
·       Biblia inasema “ Mmoja hufukuza elfu, wawili makumi elfu!”
·       Wakutanikapo wawili au watatu mimi nipo hapo katikati yao.
·       Ukiwa na tabia 6 utajenga mahusiano mazuri
·       Tabia hizi ni kama CEMENT za kuunganisha matofali ili kujenga nyumba
·       Zikikosekana ni sawa na kupanga matofali bila cement.
·       Ziko tabia 6 za lazima zinazotumika kote kote, kwenye ushirika na Mungu, Mke au Mume na hata kwa watu wote:-

1.  Tabia ya UADILIFU na UTAKATIFU
·       Ili kujenga ushirika na uhusiano mzuri UADILIFU na UTAKATIFU ni tabia za lazima.
·       Kwenda sambamba na mnayowaza na kusema kwa pamoja.
·       Kama kuna ahadi inabidi kutimiza ahadi
·       Kutawafanya kuaminiana na kuimarisha umoja na uhusiano wenu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU
(1Petro 1:15) Bali kama aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote.
v Utakatifu ndio tulioitiwa.
v Dhambi ndiyo iliyotutenga na Mungu
v Kutakaswa na kudumu katika utakatifu kutadumisha uhusiano wetu na Mungu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME
>> Uadilifu hujenga na kukuza mahusiano
>> Uovu na kusalitiana kwenye ndoa hata kama ni kwa siri, huvunja na kuua ushirika wenu. Ni kubomoa nyumba yenu kwa mikono yenu wenyewe. Mmejiloga wenyewe. Msitafute mchawi.



KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE
v Watu hupenda mtu mwadilifu
v Humwamini mtu wa jinsi hiyo kwa kila kitu.


2. Tabia ya UKWELI na UWAZI
·       Tabia ya kuficha ukweli na uongo vinavunja Ushirika na urafiki.
·       Weka vitu vyote kwenye karatasi nyeupe mbele za watu wavielewe wavione.
·       Kama mmoja ana vitu asivyopenda kwa mwingine mawasiliano lazima yafanyike tena kwa heshima na taratibu ili kulinda umoja, kuliko kuweka moyoni

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU
>> Ukweli utampendeza Mungu
>> Kuwa wazi mbele za Mungu kutaongeza kupendwa na Mungu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME
>> Mume au mke huchukizwa sana na vitu vinavyotendeka chini chini visivyoeleweka.
>>Mfano: Jamaa mmoja alimsave mpenzi wa nje kwenye simu yake kama Battery Low! Na mlio akauchagulia. Kila ikiita mke wake akiona Battery Low anaizima na kuiweka kwenye chaji. Uongo wa jinsi hii huharibu mahusiano kabisa, huna utakalojitetea mke au mume akakuamini tena.
>> Ukiwa mkweli na muwazi kwa mwezi wako utadumisha uhusiano wenu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE
>> Mtu mkweli na muwazi hupendwa na watu wote.

3. Tabia ya KUBADILIKA
·       Ukikubali kuwa hujakamilika, kwenye ushirika jipange KUBADILIKA
·       Kama kuna kitu hakijaenda vizuri angalia kama inakupasa UBADILIKE.
·       Badala ya kulaumiana jifunze kukubali KUBADILIKA.
·       Tabia ya kubadilika hukuweka uende sawa na sambamba na kukubalika.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU
v Mungu anatarajia mabadiliko makubwa unapoendelea kumjua.
v Maana ya kukua kiroho ni kuongezeka na kubadilika kuelekea ukamilifu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME
>> Badilika unapogundua umekosea.
>> Badilika unapogundua mwenzako habadiliki.
>>Tumelelewa kwenye mazingira tofauti. Mila tofauti. Desturi tofauti.
>>Lipo jambo ambalo likitendeka kwa mwingine ni furaha, na kwa mwingine ni kero. Mfano: Kubanja. Ukiona kunamkera mwenzako BADILIKA anza kuona si tendo zuri.
>> Kubadilika kutawafanya mzidi kufanana na kuongeza utulivu kwenye ndoa.
>>Badilika unapoona misimamo yako haijengi.
(Epuka misimamo mikali, mimi nimeshasema basi… Siongei tena…n.k.)

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE
>> Mungu anatarajia mabadiliko makubwa unapoendelea kumjua.
>> Maana ya kukua kiroho ni kuongezeka na kubadilika kuelekea ukamilifu.

4. Tabia ya KUSAMEHE NA KUTUBU
·       Kukiri kosa na kuomba msamaha kunawashinda wengi
·       Au kusamehe baada ya kuomba msamaha ni kazi ngumu kwa wengi
·       Tabia ya kusamehe na kutubu ili usamehewe hujenga mahusiano kwa upya
·       Ukijizoeza kutubu kutakufanya urekebishe makosa uliyofanya
·       Kutubu na kusamehe kunahitaji unyenyekevu wa hali ya juu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU
>> Kutubu hurejesha uhusiano wako na Mungu kwa upya.
>>Kuwasamehe wengine huimarisha uhusiano wako na Mungu na kuondoa kila kunyanzi moyoni.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME
>> Kosa linapotendeka, msamaha huhitajika kutoka pande zote mbili.
>>Kutokukiri makosa huharibu uhusiano kati ya mke na mume
>>Hata kama huoni kosa, na mwenzako analiona ni vema kuomba msamaha ili kurejesha uhusiano mzuri uliokuwepo, unaweza kugundua baadaye kuwa ulikuwa unakosea.  
>>Makosa yasiwe sababu ya kuwafarakanisha na kuharibu uhusiano wenu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE
>> Tabia ya kusamehe na kuomba msamaha kwa watu wote ni ya msingi katika kujenga mahusiano mazuri na watu.
>> Kutubu na kusamehe kunasaidia kuliweka wazi kosa na kuanzisha jitihada za kutolirudia badala ya kujenga ukuta wa kujilinda kwamba hujakosea, ni bahati mbaya


5.  Tabia ya HESHIMA na NIDHAMU
·       Ukitaka kuvunja kabisa uhusiano na mtu, onyesha unamdharau
·       Kila mtu anapenda kuheshimiwa
·       Dharau huharibu na kuvunja kabisa umoja na ushirika

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU
>> Mungu anapenda kuheshimiwa
>>Mungu atazidi kukupenda unapoonyesha nidhamu na heshima kwake

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME
(1Petro 3:7) Mpe mke heshima…kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
>> Heshima si kwa mume peke yake. Tunza heshima ya mke pia.
>>Kuheshimiana kunajenga umoja na mahusiano.
>>Tabia hii ya kuheshimiana hulinda na kuimarisha uhusiano wenu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE
>>Ukiwaheshimu watu wote wakubwa kwa wadogo, utajijengea uhusiano mzuri na watu wote.

6. Tabia ya KUTOA /KUJITOA
·       Tatizo kubwa la msingi au SUMU  ya ushirika ni UBINAFSI.
·       Ubinafsi ni uchawi unaologa na kuusambaratisha umoja na ushirikiano
·       Kwenye mahusiano au ushirika usisubiri wewe tu upewe, tafuta nafasi ya kutoa

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU
>>Yeye alimtoa Kristo.
>>Mungu ametupa vyote tulivyonavyo, sisi ni mawakili tu.
>>Unatazamiwa ujitoe zaidi na umtolee zaidi kuonyesha kiasi gani unampenda.



(Mwanzo 22:15-18) IBRAHIM AKIMTOA ISAKA
Ibrahimu anamtoa Isaka, yuko tayari kumchinja Mungu akasema “Nimeapa kwa nafsi yangu, kwa kuwa umetenda neno hili; wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, 17katika kukubariki nitakubariki, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao, 18na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE /MUME
(             )  Msinyimane
>>Wote wawili uhusiano utadumu na kuongezeka zaidi kama kila upande unazingatia kutoa.
>> Zawadi ndogo ndogo na kubwa kutoka kila upande husherehesha uhusiano wenu.

KWENYE JAMII NA WATU WOTE
Utapendwa na watu, utajipatia marafiki wengi ukiwa mtoaji
(Mhubiri ) Mali ikiongezeka, walao nao huongezeka
(Luka      ) Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa kwa kipimo cha kujaa na kusukwa sukwa


SUMMARY
TABIA 6 ZA LAZIMA KATIKA KUJENGA USHIRIKA
1.    TABIA YA UADILIFU NA UTAKATIFU
2.    TABIA YA UKWELI NA UWAZI
3.    TABIA YA KUBADILIKA
4.    TABIA YA KUSAMEHE NA KUTUBU
5.    TABIA YA HESHIMA NA NIDHAMU
6.    TABIA YA KUTOA NA KUJITOA

Tabia hizi hata kama unazo, ongeza viwango vyake, utajenga ushirika na mahusiano mazuri.

Mr Gamariel Chiduo
TAG Head Office