Friday, February 10, 2012

Nini maana ya Valentine? - What is Valentine?


Nini maana ya Valentine

Jina "Valentino" Jina la Mtakatifu wa Kiroma aliye itwa Valentino
Siku ya Mtakatifu Valentino 
Siku ya Valentino hufahamika kama Siku ya wapendanao wanaiita “Valentine Day”, ni maadhimisho ya mwaka, kila tarehe 14 Februari, Watu husherehekea upendo na kuthaminiana na kujaliana kati ya watu wenye uhusiano binafsi, mara nyingi hutumika kwa mahusiano ya kimapenzi.

Asili yake: Siku hii asili yake ni baada ya wakristo wa zamani kuteswa hadi kufa kwaajili ya kuupenda Ukristo. Kihistoria Mtakatifu Valentino alitumika kama kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa mfalme Claudia, Mfalme Claudia alimkamata na kumfunga. Mtakatifu Valentino aliteswa kwaajili ya Imani yake ya Kikristo na Kufa tarehe 14 mwezi Februari, 269 AD. Kwaajili ya msimamo, imani yake na kufa kwa kutetea Ukristo Papa Gelasius aliitangaza tarehe 14 mwezi wa Februari kuwa siku ya Mtakatifu Valentino mwaka 496 AD.

Watu wanasherehekeaje siku hii?
Jinsi watu wanavyo ichukulia siku hii ni kutokana na TABIA ZAO ZILIVYO au kiasi cha hofu ya kumuogopa Mungu kilivyo. Watu wengi huichukulia Siku hii kama ni siku ya Mapenzi, Wengine hufanya kama siku ya kujenga mahusiano upya, kupatana na wapendwa wao au kufurahi na wale wanaowapenda. Ila sehemu mbaya zaidi watu huchukulia siku hii kama ni siku ya KUVANYA MAOVU NA UFUSKA, HILI NI CHUKIZO KWA MUNGU. Ni bora Tuichukulie siku hii kidini zaidi kama wahasisi wa Valentine walivyofanya. Mungu aliupenda ulimwengu na kumtoa mwanawe kama kafara ya Dhambi zetu. Ni vizuri tukitumia mda tulio nao kujitakasa na kutubu dhambi zetu. Je sisi ni nini mbele za Mungu zaidi ya wale waliokuwa wanachinjwa na kuuawa kikatili kwaajili ya kulinda imani yao? HADI PUMZI YA MWISHO WALIMTAMKA KRISTO. Tuwaenzi kwa kutenda wema tu.
SWALI: Je mambo unayoyafaya siku ya valentine, Ni kuilinda Imani hadi pumzi ya Mwisho??
UPENDO: Simaanishi Watu wasipendane, tunatakiwa  tupendane kwa upendo wa Kimungu, Upendo wa Kweli, Upendo wa Kiuaminifu. Siku hizi Upendo wa kweli ni Mgumu kwawatu wengi kwasababu mbalimbali, ikiwemo dhambi na anasa za kidunia. Swala la Uaminifu, Duh! Linapelekesha watu sana.
KAMA UNASHEREHEKEA SHEREHEKEE VALENTINE ILA USIIGEUZE KAMA WAPAGANI NA WATU WASIO NA DINI WANAVYOFANYA.
Biblia inasema kila tunapotenda dhambi moja Tunampandisha Yesu msalabani tena. MUNGU ATUSAMEHE